Hatua ya kwanza; jua kwa undani tatizo ni nini. Najua utashangaa lakini ukweli ni kwamba wengi ambao wanakuwa na matatizo huwa hawajui tatizo hasa walilonalo ni nini. Na hivyo wanapokazana kulitatua wanashindwa, kwa sababu kama hujajua kiini cha tatizo huwezi kulitatua. Mara nyingi watu wamekuwa wakiangalia madhara ya tatizo, badala ya kuangalia chanzo kikuu cha tatizo. Huwezi kutibu tatizo kwa kutibu madhara, badala yake unahitaji kuzama ndani na kujua chanzo hasa cha tatizo ni nini. Na njia ya uhakika ya kufikia hilo ni kuuliza swali moja muhimu sana, KWA NINI. Uliza swali hili mara tano, yaani uliza kwa hatua tano. Kwa mfano kama tatizo lako ni kipato kidogo kwenye biashara yako, jiulize kwa nini kipato ni kidogo, jibu linaweza kuwa wateja ni wachache, jiulize tena kwa nini wateja ni wachache, hapo utapata majibu mengine, kwa kila jibu jiulize tena kwa nini? Mpaka utafika mahali na kuona hiki ndio kiini kikuu cha tatizo. Lijue tatizo vizuri, wahenga walisema kul...
Comments
Post a Comment